Skip to main content

DC KIGOMA ASISITIZA MAADILI MEMA KWA JAMII




Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Hamis Kali  ameendelea kutoa elimu ya Kuzingatia maadili na miiko ya  Kitanzania na kuepuka Vitendo vya ukatili   

Aliyasema hayo Jana April 17, 2023 alipokuwa akihutubia Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Mtaa wa Taifa  Kata ya Rusimbi  ambapo pia alisikiliza Kerò za Wananchi pamoja na kuzitatua  

Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Wazazi kuendelea kuwaelimisha Watoto Kuzingatia maadili sahihi na kuepuka Migogoro na ukatili  ndani ya familia inayosababisha ongezeko la  watoto wa mitaani 

Aidha aliwataka Wananchi kuendelea kuhamasika  kulima zao la Michikichi ya Kisasa kwa lengo la kuwa na uzalishaji mkubwa na wenye tija ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na familia

Alisema tayari ugawaji wa kadi za vitambulisho vya Taifa (NIDA) unafanyika kwa kila Kata kwa Wataalamu kupita kugawa kwa kuhirikiana na viongozi wa eneo husika 

Naye Diwani wa Kata ya Rusimbi Mhe. Bakari Songoro akiishukuru Serikali ya Awamu ya Sita 

kwa niaba ya Wananchi kwa Utekelezaji wa miradi  alisema Serikali imekamilisha Ujenzi wa wodi ya Wazazi  katika Zahanati ya Rusimbi kwa gharama ya Tsh 76, 765, 000/= na tayari inafanya kazi 

Alisema Serikali imeboresha Ujenzi wa vyumba  vya Madarasa matatu (03) Katika Shule ya Sekondari Rusimbi kwa gharama ya Tsh 60, 000, 000/= , Uboreshaji wa maabara ya Shule kwa gharama ya Tsh 20, 000, 000/= na ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Kipampa.


Chanzo: @kigomaujijimc

Comments

Popular posts from this blog

GET TO KNOW EXTENDED MARKERTING MIX

The extended marketing mix is, as the name suggests, an extension of the marketing mix which was traditionally for products. The 4P’s are also known as product marketing mix. As services came more into the picture it was seen that the 4p’s could not justify the marketing mix. There were 3 more elements which were necessary to actually explain the marketing of services. When products began offering services, the extended marketing mix began applying to products as well (like Maruti service stations where Maruti is a product and the service station is a service). These are the elements which were added to the marketing mix to form the extended marketing mix. In the above figure, the product marketing mix are the first four P’s and the next 3 P’s are added to make the Extended Marketing mix. This extended marketing mix is also known as the service marketing mix. The four PS mainly constituted the following 4 elements Product Price Place Prom...

7 BUSINESS LOCATION THAT INCREASE BRAND VISIBILITY

Marketing has changed and it has become more personal. People nowadays need convenience and you cannot expect that your customer will come to you. You will have to go to your customer again and again so that he does not switch to any other brand. Remember that your customer has numerous options in his hand. Thus your business needs to present in locations where the customer can make his buying decision easily. This is where your business location plays an important role. The process of managing a business is continually changing but more importantly with the advent of online marketing, your business location itself has changed. Because of the increasing usage of internet, Smart phones too are the latest trend and hence the reach of internet is now quadrupled. But it is not necessary that your customer be present only on the internet. Brick businesses are as alive today as online businesses. Below you will find a list of 7 business locations that you should be ...

TISS YAPATA BOSS MPYA.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Amemteua Bw.Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa taifa,Kuchukua nafasi ya Kamishina Diwani Athuman Msuya  Ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya Uteuzi huo Bw.Masoro alikua akihudumu katika Idara ya Usalama wa Taifa kama Naibu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa shughuli za  ndani wa Usalama wa Taifa. Wakati huo huo Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga Kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, Nchini Marekani na muwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa. Balozi Katanga anachukia nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston,Ambaye Uteuzi wake umetenguliwa. Balozi Katanga kabla ya Uteuzi huu alikua Katibu Mkuu Kiongozi. Vile vile Mhe.Rais Dkt.Samia amemteua Bw.Moses Mpogole Kusiluka Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi,Ambapo kabla ya Uteuzi huo alikua Katibu Mkuu Ikulu. Taarifa Rasimi Kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu iliyotolewa mapema Jana Januari 3,2023, i...