Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Amemteua Bw.Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa taifa,Kuchukua nafasi ya Kamishina Diwani Athuman Msuya Ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya Uteuzi huo Bw.Masoro alikua akihudumu katika Idara ya Usalama wa Taifa kama Naibu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa shughuli za ndani wa Usalama wa Taifa. Wakati huo huo Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga Kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, Nchini Marekani na muwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa. Balozi Katanga anachukia nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston,Ambaye Uteuzi wake umetenguliwa. Balozi Katanga kabla ya Uteuzi huu alikua Katibu Mkuu Kiongozi. Vile vile Mhe.Rais Dkt.Samia amemteua Bw.Moses Mpogole Kusiluka Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi,Ambapo kabla ya Uteuzi huo alikua Katibu Mkuu Ikulu. Taarifa Rasimi Kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu iliyotolewa mapema Jana Januari 3,2023, i...
Comments
Post a Comment