Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amekutana na kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge wa majimbo ya mkoa wa Kigoma.
Waziri Kairuki amekutana nao Februari , 2023 Jijini Dodoma kwa lengo la kuzungumza, kushauriana na kupata mwelekeo wa pamoja katika changamoto zinazowakabili wananchi hasa katika upatikanaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo huduma ya afyamsingi, elimu, miundombinu ya barabara na utawala.
Mhe. Kairuki amesema ninyi ndio wawakilishi wa wananchi wetu wa Mkoa wa Kigoma tunaamini haya tunayojadili ndio changamoto za wananchi hivyo Ofisi ya Rais- TAMISEMI ipo tayari kushirikiana nanyi tunaamini kwa pamoja tutaweza kutatua changamoto hizi za wananchi"
Waziri Kairuki ameendelea na utaratibu wa kukutana na Waheshimiwa Wabunge kwa lengo la kuzungumza nao kwa pamoja kuona ni namna gani watashirikiana katika upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Chanzo: @ortamisemi@Kigoma Press Club kgpc
Comments
Post a Comment