Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2023

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WADAU WA ZAO LA CHIKICHI

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiongoza kikao kazi kilichomkutanisha na wadau wa Kilimo cha zao la chikichi mkoani Kigoma. Awali akifungua kikao hicho, Waziri Mkuu amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kufanya Tathimini ya Mafanikio yaliyofikiwa katika kuibua, kuendeleza na kuboresha kilimo cha zao la chikichi mkoani Kigoma Kikao kazi hicho kinafanyika katika Ukumbi wa NSSF Manispaa ya Kigoma-Ujiji na kuwakutanisha Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, wazalishaji wa mbegu za chikichi, wamiliki wa viwanda vidogo vya kuchakata zao hilo pamoja na wakulima wakubwa na wadogo wa chikichi mkoani hapa. CHANZO:Kigoma Press Club Kgpc

WAZIRI MKUU AZITAKA TAASISI ZA MAAFA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU

  Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa amezitaka sekta zote zinazohusika na utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa maafa, idara au taasisi zenye jukumu la kisheria la kutekeleza kazi hiyo zihakikishe zinawajibika kikamilifu katika kushughulikia vizuri pindi maafa yanapotokea. Amesema pamoja na uwepo wa sera na sheria ya usimamizi wa maafa na nyaraka alizozindua ambazo zimelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji kwa kila sekta, ushirikiano unahitajika katika kutekeleza afua za ustahimilivu na kukabiliana na maafa. Ameyasema hayo (Alhamisi, Februari 9, 2023) wakati akizindua nyaraka za usimamizi wa maafa katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. Nyaraka zilizozinduliwa ni Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na kukabiliana na Maafa (2022). Nyaraka nyingine ni Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano Wakati wa Maafa (2022), Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja (2022-2027), Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (2022-2027) na Mwongozo wa Taifa wa Kupambana na Vitendo vya Kihali...

MHE. KAIRUKI AKUTANA NA WABUNGE WA MAJIMBO YA MKOA WA KIGOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki  amekutana na kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge wa  majimbo ya mkoa wa Kigoma. Waziri Kairuki amekutana nao Februari , 2023 Jijini Dodoma kwa lengo la kuzungumza, kushauriana na kupata mwelekeo wa pamoja katika  changamoto zinazowakabili wananchi  hasa katika upatikanaji wa huduma kwa wananchi  ikiwemo huduma ya afyamsingi, elimu, miundombinu ya barabara na utawala. Mhe. Kairuki amesema ninyi ndio wawakilishi wa wananchi wetu wa Mkoa wa Kigoma tunaamini haya tunayojadili ndio changamoto za wananchi  hivyo Ofisi ya Rais- TAMISEMI ipo tayari kushirikiana nanyi tunaamini kwa pamoja tutaweza kutatua changamoto hizi za wananchi" Waziri Kairuki ameendelea na utaratibu wa kukutana na Waheshimiwa Wabunge  kwa lengo la kuzungumza nao kwa pamoja kuona ni namna gani watashirikiana katika upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi. Chanzo: @ ortamisemi@Kigoma Press Club kgpc