Kwa
mara ya kwanza katika jiji la mwanza yale mashindano ya michezo
mbalimbali yanayohusisha vyuo vikuu nchini Tanzania yakihusisha michezo
ya mpira wa miguu,(football), Mpira wa wavu(volleyball) Riadha pamoja na
Urimbwende yamefanyika katika jiji la mwanza.
Mashindano
hayo yaliyovuta hisia za wakazi wa jiji la mwanza yalihudhuliwa na
mamia ya wakazi wa jiji hili ili kupata kujionea vipaji katika michezo
mbalimbali iliyo husisha vyuo vyote vya jiji la mwanza vikiwemo,SAUT
Bugando,CBE,Chuo cha Mipango,na vingine vingi vyote vya jijini mwanza.
Mashindano
haya yaliandaliwa na kampuni ya kampuni ya Tanzania Eleveted Greean
company limited ikishirikiana na Nyanza Communication Cosultancy
Limited ya jijini mwanza chini ya udhamini wa SBS Tanzania kama
mdhamini mkuu na Clouds Media Group.wadhamini wengine walikuwa ni Mama
Raja Decorations, Millenium Park Hotel, Clara Saloon pamoja na Flora
saloon zote za jijini Mwanza
Katika
utangulizi wa mashindano hayo michezo ya mpira wa miguu,riadha,mpira wa
wavu vilifanyika katika uwanja wa CCM kirumba mwanza,na kufuatiwa na
mashindano ya ulimbwende yaliyomalizikia pale katika ukumbi wa Villa
Park Resort kwaajiri ya kumpata mrembo wa vyuo vikuu kanda ya mwanza na
washindi kutangazwa siku hiyohiyo ya tarehe 7/6/2013.
Washindi
katika mchezo wa football walikuwa ni BASO SAUT,katika volyball mshindi
alikua ni SAUT East,katika riadha mshindi wa kwanza alitoka SAUT pia
akijulikana kwa jina la Axweso Yeremia na katiaka ulimbwende SAUT tena
ilivibwaga chini vyuo vingine kwa mshiriki Reginamary Ngurendo kuibuka
na ushindi akifuatiwa na Stela Charles kutoka Chuo cha Mipango Mwanza.
 |
Miss Inter university Regnamary akiielezea furaha yake baada ya kutwaa taji hilo. |
 |
Washiriki katika moja ya maonesho ya kuonesha vipaji katika kuusakata muziki |
 |
Happy na pendo kama majaji wakiwa kazini. |
 |
Mapozi ya twiga yakahusika pale kati |
 |
Naomba mic niseme chochote...... |
 |
Kiafrica tumependeza hatujapendeza??? |
 |
Vazi la beach hapo sasa...... |
 |
Umeniona na mikato yangu |
 |
Hapo vip....? |
 |
Baadhi
ya waandaaji wa shindano hilo kutoka Nyanza Communication Consultancy
Limited wakiwa na mmoja wa wawakilishi kutoka SBS Tanzania katika picha
ya pamoja katika red carpet. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
 |
BAADHI YA TIMU SHIRIKI KUTOKA VYUO MBALIMBALI VILIVYOPO KATIKA JIJI LA MWANZA |
 |
MASHABIKI WAKIFANYA YAO. |
 |
Timu kutoka mipango |
 |
kiduku kikahusika kinomanoma pale kirumba |
 |
Mshindi wa mbio za kilometa 10 bwana Axweso Yeremia kutoka SAUT mwanza. |
 |
timu kutoka CBE |
Comments
Post a Comment