Waziri wa ushilikiano wa Afrika Mashariki Mh.Samweli Simwanza Sita amewaasa vijana nchini kuwa wazalendo kwa nchi yao ili kuendana na ushindani uliopo katika soko la Ajira katika ukanda wa Afrika mashariki.
Waziri Sitta aliyasema hayo katika mahafali ya nne ya chama cha wanafunzi wanaosoma mahusiano ya uma katika chuo cha mtakatifu Agustino,Saut Students Public Relations Association (SSPRA). Katika mahafari hayo makamu mkuu wa chuo Dr.Charles Kitima alieleza changamoto zinazolikabili taifa ikiwemo ukosefu wa Ajira miongoni mwa vijana hasa wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
Makamu mkuu wa chuo Dr.Charles Kitima alikemea vitendo vya watawala kujali maslahi yao binafsi pasipo kujali masilahi ya wananchi waliowapa dhamana ya kuwaongoza.
Aidha waziri Sitta alisisitiza uadilifu na weledi katika utendaji wa kazi ili kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii wanayo kwenda kuitumikia.
|
Mgeni rasimi katika mahafari ya SSPRA Mh.Waziri Samweli sitta akifurahia jambo na makamu Mkuu wa chuo Dr.charles Kitima (kulia) na mtaaluma mkuu mh.Dr.thadeus Mkamwa |
|
Makamu mkuu wa chuo Dr.Kitima akisitiza jambo. |
|
Waziri wa Ushirikiano wa Africa mashariki Mh.samweli Sitta akiwaasa wahitimu kuzingatia taaluma na weledi katika kuihudumia jamii |
|
Mwenyekiti mstaafu Ndugu Christopher Ngonyani na Mlezi mwanzilishi Ndugu Albert Tibaijuka |
|
Mwenyekiti mstaafu wa kamati ya maadili na weledi ndugu Anthonius Clement katika tafrija hiyo |
|
picha ya pamoja Kutokatoka kushoto ni Damali Machaku katikati Severina Kayuni na Anthonius Clement |
Comments
Post a Comment