Skip to main content

JESHI LA POLISI LATANGAZA AJIRA KWA MWAKA 2012/2013 KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA VYUO

TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013.Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili. Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013.Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi kujaza fomu za maombi zinazopatikana kwenye tovuti ya Polisi kwa anuani www.policeforce.go.tz www.policeforce.go.tzFomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013 kwa:

Inspekta Jenerali wa Polisi,

Makao Makuu ya Polisi,

S.L.P. 9141,

DAR ES SALAAM.

Fani zinazotakiwa ni; Shahada za Menejimenti ya Rasilimali watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLE), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi(Educational Psychology and Councelling),Takwimu, Lugha(Kiswahili/Kiingereza/Kifaransa/Kireno/Kiarabu), Usimamizi wa Programu za Maendeleo ya Jamii, Uhusiano wa Kimataifa, Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering), Uhandisi Kompyuta(Net Work, System Analyst, Data Base, Electronic & Telecommunications), Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma, Upangaji na Uendeshaji miradi, Jinsia na Watoto. Pia stashahada katika Usimamizi wa programu za maendeleo ya Jamii, Utunzaji kumbukumbu na Ukutubi.

Sifa za Muombaji:

  • Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Awe na umri usiozidi miaka 28.
  • Awe na tabia njema.
  • Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa la jinai.
  • Awe na afya njema.
  • Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
  • Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Asiwe na alama za kuchora mwilini(Tatuu).
  • Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya na
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya Polisi.

Imetolewa na:

Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,

Makao Makuu ya Polisi,

S.L.P. 9141,

DAR ES SALAAM.

Comments

Popular posts from this blog

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE.

 “MANENO PINGAMIZI YASIKWAMISHE UAMSHO WAKO BINAFSI” (2) Siku ya Pili 28, Aprili 2022  Semina ya Neno la Mungu - Dodoma LINK YA SOMO LA HILI YOUTUBE 👉🏼 https://youtu.be/Rwo70MEHQd0    NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA 👉🏼https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda  UTANGULIZI LENGO YA SOMO ➖Uamsho kutoka kwa Mungu uliokusudiwa kwa ajili yako uweze kuupata majira haya nyakati hizi. Wasomaji wa Biblia, historia ya ulimwengu na kanisa wanajua kabisa kipindi chochote kinachotangulia matatizo, kinachofuata ni maombi na baadaye unafuata uamsho. Kama kuna tatizo limepita katika taifa, ujue kuwa kuna watu watainuka kuomba kwa ajili ya lile taifa, na matokeo yake ni uamsho katika lile taifa. Hili lipo katika kanisa, familia na mahali pengine popote. Msisitizo wa somo hili ni ujue namna ya kufanya wakati Mungu anaachilia uamsho huu katika nyakati hizi, maneno pingamizi yasiwe kikwazo kwako. Pia ujue kitu cha kufanya katika kupokea uamsho huu. Uamsho unaanza na mtu bin...

GET TO KNOW WHAT IS INTERNENT

What is Internet The internet in simple terms is a network of the interlinked computer networking worldwide, which is accessible to the general public. These interconnected computers work by transmitting data through a special type of packet switching which is known as the IP or the internet protocol. Internet is such a huge network of several different interlinked networks relating to the business, government, academic, and even smaller domestic networks, therefore internet is known as the network of all the other networks. These networks enable the internet to be used for various important functions which include the several means of communications like the file transfer, the online chat and even the sharing of the documents and web sites on the WWW, or the World Wide Web. It is always mistaken said that the internet and the World Wide Web are both the same terms, or are synonymous. Actually there is a very significant difference between the t...

GET TO KNOW EXTENDED MARKERTING MIX

The extended marketing mix is, as the name suggests, an extension of the marketing mix which was traditionally for products. The 4P’s are also known as product marketing mix. As services came more into the picture it was seen that the 4p’s could not justify the marketing mix. There were 3 more elements which were necessary to actually explain the marketing of services. When products began offering services, the extended marketing mix began applying to products as well (like Maruti service stations where Maruti is a product and the service station is a service). These are the elements which were added to the marketing mix to form the extended marketing mix. In the above figure, the product marketing mix are the first four P’s and the next 3 P’s are added to make the Extended Marketing mix. This extended marketing mix is also known as the service marketing mix. The four PS mainly constituted the following 4 elements Product Price Place Prom...