Ripoti Maalum:Wizi wa fedha katika ATM ulivyofanyika
Taarifa
za wizi huu zilianza kurindima Machi 2010 na Sh300 bilioni ziliibwa kwa
njia ya mtandao kupitia mashine za ATM, kati ya kiasi hicho Sh360
milioni zikihusisha benki moja ya NBC.
Hata hivyo, mwaka huo walikamatwa watu wanne baada ya kuripotiwa wizi huo mkubwa, sambamba na taarifa za kukamatwa kwa watu hao alikamatwa mfanyabiashara mmoja aliyefanya jaribio la kuiba Sh221 milioni kutoka Benki ya NBC.

Wimbi
la wizi huo limeibuka tena Oktoba mwaka jana hadi Februari mwaka huu,
inakadiriwa Sh700 milioni zimeibwa Benki ya NMB na benki zingine kwa
nyakati tofauti.
Tayari,
polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB
wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu wanne ambao wanadaiwa kukutwa wakiwa
kwenye mpango wa kuendelea kuiba fedha ndani ya mashine za kuchukuliwa
fedha (ATM) za Benki ya NMB tawi la PPF Plaza, saa 6:00 usiku.
Kunaswa
kwa watu hao kunatokana na mtego baina ya maofisa wa benki na polisi
uliofanikisha Februari 10 mwaka huu, kumtia mbaroni mtuhumiwa mmoja
akiwa katika ATM ya NMB katika tawi la PPF Plaza, akiingia kuchukua
fedha ambaye alifanikisha kunaswa kwa watuhumiwa wengine na vifaa
vinavyotumika kwa wizi huo.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Christopher Fuime alieleza kuwa baada
ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo alifanikisha kukamatwa wengine, ikiwamo
vifaa mbalimbali ambavyo wamekuwa wakivitumia kufanyia uhalifu huo.
“Kwa
muda mrefu sasa tulikuwa tukihangaika na wahalifu wa aina hii, kwani
tangu mwaka Oktoba mwaka jana tumekuwa tukipokea kesi mbalimbali za wizi
wa fedha katika akaunti zao, lakini tumefanikiwa juzi kuwatia mbaroni,”
alisema.
Tangu
kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao, idadi ya malalamiko ambayo wastani
wa kesi 15 walizokuwa wakipokea kwa siku 14 zimeisha, hali ambayo
inawafanya kuamini kuwa wahusika hao walikuwa vinara wakuu wa wizi huo.
“Hatuna
maana kwamba kukamatwa kwao uhalifu huu utapungua, wizi huu una
mtandao mpana kwa vile hata wahalifu hao wamedokeza wamekuwa wakifanya
uhalifu huo kwa kushirikiana na wataalamu wa kompyuta kutoka nchini
Bulgaria,” alisema.
Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa vilivyokamatwa ni kadi bandia za kuchukulia fedha katika ATM 194 za Banki ya NMB, kati yake kadi 95 zilikuwa na namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina na picha ya mtu anayedaiwa ni mtumiaji, kadi zingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti namba 5068000322 zikitumia jina lingine na picha moja.

Pia,
walinasa kadi za Benki ya DTB 36, ambazo kati yake 18 zilikuwa na jina
moja la Kelvin G. Gratias zikiwa namba 20497883, kadi 12 zikitumia jina
lingine na akaunti namba 2049783, huku kadi sita zikitumia jina la mtu
mwingine akaunti namba 2049783.
Kadi
zingine tatu zenye maandishi ya Download List na nyingine ikiwa ni kadi
ya visa ya Benki ya KCB yenye namba 4183546040003827 zikitumia jina
moja, kadi zingine zilikuwa ni tupu zisizo na maandishi wala nembo ya
benki yoyote na nyingine zikiwa na nembo ya Soviet Royality, kadi ya
raia wa Urusi ikiwa na namba Sand 000724.
source: ww.mwananchi.co.tz
Comments
Post a Comment