Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2023

WANANCHI WAASWA KUFANYA MAZOEZI KUIMARISHA AFYA.

Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa, amewaasa  wananchi Wilayani humo kujenga tabia ya kufanya Mazoezi na kushiriki Michezo mbalimbali Ili kuimarisha afya na kuepuka magonjwa mbali mbali. Kanali Mallasa ametoka wito huo,wakati wa kikao Cha sherehe za kukaribisha mbio za Mwenge kilichofanyika tarehe 18,Julai,2023 katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya Kakonko. "Niwaombe Kila mkuu wa Idara  Taasisi hata Mwananchi mmojammoja  Kwa pamoja,kujitokeza kushiriki Mazoezi Ili kuimarisha afya na kuepukana na Magonjwa mbalimbali ambayo tiba yake inaweza Kuwa ni Mazoezi tu"ameeleza Kanali Mallasa Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko,Bw.Ndaki Stefano Mhuli,Amesema uongozi wa Halmashauri unatambua umuhimu wa Mazoezi na michezo kwa ujumla,hivyo umetenga siku ya Jumamosi kama siku maalum kwaajiri ya Watumishi wa Halmashauri kushiriki Mazoezi na Michezo,Ili kuimarisha afya zao. "Mhe.mkuu wa Wilaya niseme tu Jambo hili tunalichumilia kwa uzit...

ZIARA YAKUKAGUA MIRADI INAYOTARAJIWA KUZINDULIWA NA MBIOZA MWENGE MWAKA HUU

  Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa,amewataka wataalam,wanaosimamia na kuratibu miradi mbali mbali ya maendeleo inayo tarajiwa Kuzinduliwa na Mbio za mwenge mapema mwezi Agosti Mwaka huu,kuhakikisha wanamaliza changamoto zilizobakia katika miradi hiyo ambayo itazimduliwa na mbio za Mwenge Wilayani Kakonko. Wito huo umetolewa  Julai 12,2023 wakati wa ziara ya kukagagua miradi hiyo inayoendelea  kutekelezwa. "Ndugu zangu,muda uliobaki wa kukamilisha na kuondoa dosari ndogo ndogo zilizopo ni Mchache kabla ya Ujio wa Mwenge wa Uhuru Wilayani kwetu,niwatake wataalamu wote wanaohusika na miradi hii,kujitahidi kuondoa changamoto tunazoziona,Ili kuepuka miradi kukataliwa na viongozi wa Mbio za Mwenge....itakua ni fedheha Kwa Wilaya na mkoa kwa ujumla kwani taswila halisi ya mkoa wa kigoma katika mbio za Mwenge mwaka huu itaonekana  Kuanzia Wilayani Kakonko"Alisema Kanali Mallasa. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko Bw.Ndaki Stefano Mhul...