Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Aggrey Magwaza amefanya kikao cha kwanza cha Kamati ya maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 na kupitisha miradi itakayopitiwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru utakaokimbizwa Wilayani Kakonko tarehe 16 Agosti, 2023. Col. Aggrey Magwaza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo anayekaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko amekutana na wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko leo Mei 17, 2023. Miradi iliyopendekezwa na kupitishwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023 ni Uzinduzi wa vyumba 08 vya madarasa na ofisi 3 za waalimu shule ya Sekondari ya wasichana Kakonko, Kutembelea kikundi cha Vijana bodaboda Muganza, Uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala kikundi cha Vijana Itumbiko, Kuweka jiwe la Msingi nyumba ya Mkuu wa Wilaya (Ikulu ndogo Kakonko) inayojengwa Itumbiko, Kukagua Barabara ya lami Kakonko-Itumbiko inayoelekea hospitali ...