Na. A.C KUZENZA Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mallasa,amewaasa vijana Wilayani Kakonko kuzingatia maadili mema yenye kulinda utu wa mtu na kuzingatia maadili ya kiafrika hususani yale ya Kitanzania. Ametoka Wito huo Leo Ijumaa Aprili 21,2023 wakati wa Sherehe za Mahafali ya 1 ya Chuo Cha Elimu ya Ufundi Stadi JKT Kasanda, kilichopo Wilayani Kakonko mkoani kigoma. Akiwahutubia wahitimu hao,Kanali Mallasa,amewataka vijana hao kuyatumia mafunzo waliyoyapata chuoni hapo kutumia fursa za miradi inayotekekezwa Wilayani Kakonko kupunguza Uhaba wa mafundi katika Fani mbali mbali jambo linalopelekea Wilaya kutafuta Mafundi Kutoka nje ya Wilaya jambo linalo pelekea kudumaza Uchumi wa Watu wa Kakonko. "Wilaya ya Kakonko tunao uhitaji mkubwa wa mafundi wa fani mbalimbali,hali inayopelekea kutafuta mafundi kutoka nje ya Wilaya yetu,Kwa uwepo wa chuo hiki naiona changamoto hii inakwenda kupungua" Alisema Kanali Mallasa Aidha Amewasisitiza w...