Skip to main content

BURIANI BI.KIDUDE

Mwimbaji nguli wa muziki wa tarabu nchini Tanzania Fatma binti Baraka, maarufu kama Bi Kidude amefariki Jumatano kisiwani Zanzibar akiwa na umri wa zaidi ya miaka 100.
Taarifa ya kifo chake ilitolewa na mjukuu wake Fatuma Baraka ambaye pia ni muimbaji wa Taraabu. Alisema Bi Kidude alifariki hospitalini kutokana na maradhi ya kisukari na uvimbe kwenye Kongosho.

Bi Kidude amekuwa katika fani ya muziki wa taarab ya kiasili pamoja na ngoma za unyago kwa zaidi ya robo tatu ya umri wake.
Katika miaka ya karibuni afya yake imekuwa ikizorota kiasi cha serikali ya Zanzibar kumzuia kupanda majukwaani kuburudisha japokuwa alionekana katika tamasha la Sauti za Busara mwezi Februari mwaka huu.
Mipango ya mazishi ya nguli huyu inafanywa nyumbani kwake Zanzibar.
Wengi, hasa vijana wa kizazi kipya wanamfahamu Bi. Kidude kwa uwezo wake mkubwa wa kuimba taarabu kwa kuchanganya lugha ya kiswahili na ile ya kiarabu. Nyimbo zake za kiarabu mara nyingi zimekuwa na ladha kama ile ya aliyekuwa mwimbaji gwiji wa Misri Ummu Kulthumu.
Sio uimbaji tu uliomfikisha Bi. Kidude alipofika, bali uwezo wake pia wa kutunga mashairi, kutumia ala za mziki kama vile kupiga ngoma na hata ngoma za unyago, vyote hivi vilimuweka Bi. Kidude katika nafasi tofauti katika jamii.
Alikuwa na tabia ya kumwita kila mtu 'mwanangu,' ingawa yeye mwenyewe hakubahatika kupata mtoto. Katika mahojiano aliyofanyiwa na vyombo mbali mbali vya habari, mwenyewe alisikika akisema, ingawa alikuwa na hamu ya kupata mtoto, lakini Mwenyezi Mungu hakumjaalia.
Katika miaka ya hivi karibuni, Bi. Kidude alishirikishwa sana na wasanii wengine katika kazi zao. Miongoni mwao ni Ahmada Amelewa, Fid Q Juhudi za Wasiojiweza.
Mbali na hayo, mashirika mbali mbali yakiwemo ya kibiashara na yale yasiyo ya kiserikali yaliona mvuto aliokuwa nao Bi. Kidude katika jamii, hivyo wakamtumia katika matangazo mbali mbali maarufu likiwa lile la kutokemeza Malaria.
Ni bibi aliyebahatika kusafiri takriban duniani kote, na vilevile katika maisha yake alijinyakulia tuzo lukuki. Miongoni mwa hizo ni ile ya 2005 WOMEX ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki.
Katika siku zake za mwisho, Bi. Kidude alikuwa akiumwa, lakini wengi wanahusisha kuumwa kwake na utu uzima aliokuwa nao.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa wote, lakini zaidi ni wanamziki wa kizazi kipya waliokuwa wakimuona Bi. Kidude ni nyanya yao.

 kwa hisani ya www.bbc swahili.co.uk

Comments

Popular posts from this blog

7 BUSINESS LOCATION THAT INCREASE BRAND VISIBILITY

Marketing has changed and it has become more personal. People nowadays need convenience and you cannot expect that your customer will come to you. You will have to go to your customer again and again so that he does not switch to any other brand. Remember that your customer has numerous options in his hand. Thus your business needs to present in locations where the customer can make his buying decision easily. This is where your business location plays an important role. The process of managing a business is continually changing but more importantly with the advent of online marketing, your business location itself has changed. Because of the increasing usage of internet, Smart phones too are the latest trend and hence the reach of internet is now quadrupled. But it is not necessary that your customer be present only on the internet. Brick businesses are as alive today as online businesses. Below you will find a list of 7 business locations that you should be ...

GET TO KNOW WHAT IS INTERNENT

What is Internet The internet in simple terms is a network of the interlinked computer networking worldwide, which is accessible to the general public. These interconnected computers work by transmitting data through a special type of packet switching which is known as the IP or the internet protocol. Internet is such a huge network of several different interlinked networks relating to the business, government, academic, and even smaller domestic networks, therefore internet is known as the network of all the other networks. These networks enable the internet to be used for various important functions which include the several means of communications like the file transfer, the online chat and even the sharing of the documents and web sites on the WWW, or the World Wide Web. It is always mistaken said that the internet and the World Wide Web are both the same terms, or are synonymous. Actually there is a very significant difference between the t...

1️⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA WAJENZI-DODOMA : NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE

1️⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA WAJENZI-DODOMA : NA MWL. CHRISTOPHER  MWAKASEGE SIKU YA KWANZA: 27 APRILI, 2022 SOMO: “MANENO PINGAMIZI YASIKWAMISHE UAMSHO WAKO BINAFSI”  UTANGULIZI LENGO YA SOMO Uamsho kutoka kwa Mungu uliokusudiwa kwa ajili yako uweze kuupata. Na msisitizo hapa haupo kwenye maneno bali upo kwenye uamsho. Na kati ya kitu kimojawapo tutakachoshughulika nacho kwenye somo hili ni maneno pingamizi ambayo yanatafuta kila namna ya kukukwamisha ili usipokee kile Mungu alichokikusudia kwako na usifike pale Mungu alipokusudia ufike.   Na kwa leo nataka tujifunze na kuangalia juu ya UMUHIMU WA UHUSIANO WA UAMSHO WAKO WA LEO NA MAFANIKIO YAKO YA KESHO   Soma Matendo ya Mitume 12:1-17 Maandiko yanasema kwenye mstari wa 7 kusema “Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.” Malaika alimwamsha Petro ili apate uamsho wake binafsi akiwa...