Watu wengi Katika Jamii Huwa hawajishugulishi na Jambo lolote Ikiwa tu limetokea Katika Jamii naJambo hilo kuonekana kutowagusa Moja kwa Moja. Hali hii Mara Zote hutegemea na tabaka la Jamii,mtu/Watu, Imani na pengine Mazingira Jamii iliyopo,Ikilinganishwa na Jambo husika lililotokea. Wakati nikiwa Mdogo baba na mama yangu walikua wakinieleza Tena kwa vitendo juu ya dhana hii ya kujisemea HAYANIHUSU,Kuna Siku nlikua nikitembea na baba kuelekea shambani Mara njiani tukakuta Mti Mdogo umeanguka njiani nilifika na kuvuka lakini Baba Yangu Akaniita na kunambia hii si Tabia njema,Maana Njia hii inatumiwa na Watu wengi ndiyo tutakayo tumia kurudi Nyumbani,Na Hatujui tutarudi Kukiwa bado na mwangaza au Usiku ukiwa umeingia, Mti Huu waweza kumuumiza mmoja wetu au watumiaji wengine wa Njia hii... Ukiutoa na Kuweka kando utaonesha kuwa Unawajali na wengine. nikapata Funzo na tangu Siku hiyo Nikajikuta nikikuta kitu Njiani kinacho weza Leta Madhara kwangu na Watu wengine siwez k...