Skip to main content

Posts

KAMATI YA SIASA YA ZURU MIRADI WILAYANI KAKONKO.

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa Kigoma,Ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa Kigoma Bw.Malima Mobutu, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kakonko,leo Juni 30,2023. Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi, Mkuu wa Wilaya Kakonko  Kanali Evance Mesha Mallasa,ameambatana na Kamati ya Usalama Wilaya  Kakonko, Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya Kakonko pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  Wilaya Kakonko. Akizungumza Wakati wa Majumuisho ya ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Mkoa Kigoma Bw.Mobutu ameeleza namna Kamati ya siasa ilivyoridhishwa na namna miradi hiyo inavyoendelea kutekelezwa Wilayani Kakonko,na amewataka watendaji kurekebisha kasoro ndogo ndogo zilizo bainika katika Miradi iliyotembelewa na miradi mingine Yote inayoendelea kutekelezwa. "Kwa niaba ya Kamati ya siasa ya Chama,nitumie Fursa hii kuwapongeza watendaji wote,na kwa ujumla nis...

WANANCHI WILAYANI KAKONKO WAHIMIZWA KUTUNZA MIUNDOMBINU.

Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa, Leo Juni,28,2023,amewaasa Wananchi  wilayani kakonko kuitunza miundombinu mbalimbali ilinayowekwa na serikali Ili kuwahudumia Wananchi.  Kanali Mallasa Ametoa wito Huo wakati akipokea daraja la Muda la Chuma lililojengwa katika mto Muhwazi Barabara ya Kakonko - Ikambi linalounganisha Shule ya Sekondari Ikambi na kata ya Kakonko mjini,ambalo Ujenzi wake umetekelezwa na kamandi ya Magharibi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na TARURA Wilaya Kakonko. Akizungumza wakati wa kupokea daraja hilo Kanali Mallasa,Amelishukuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na TARURA kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa huduma za Jamii ikiwemo Shule ya Sekondari Ikambi. Aidha Amewasisitiza Wananchi  Wilayani Kakonko hususani wa Kijiji Cha Itumbiko na kata nzima ya Kakonko kuitunza miundombinu ya daraja hillo Ili  iweze kudumu na kuwahudumia  Wananchi kwa ufanisi. "Niwaombe Wananchi Pamoja na TARURA, ...

MKUU WA WILAYA YA KAKONKO AKAGUA MIRADI 07 ITAKAYOTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU 2023.

  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya amekagua miradi 07 itakayotembelewa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2023 na kusisitiza mapungufu yaliyoonekana katika miradi hiyo kufanyiwa kazi. Col.Mallasa amefanya ziara hiyo siku ya jumatano Mei 31, 2023 akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama, Viongozi wa chama cha mapinduzi CCM (W), Katibu wa Mbunge, Wakuu wa Taasisi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri. Katika ziara hiyo viongozi walitembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko, Ujenzi wa  Wodi tatu za Hospitali ya Wilaya Kakonko, Kiwanda Cha Uzalishaji Mkaa mbadala,Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya (IKulu ndogo), Ujenzi wa Ofisi ya Afisa Tarafa Kasanda, Kikundi Cha wanunuzi wa mazao ya nafaka Kiziguzigu  Pamoja na Kituo Cha Mafuta Glory to God. Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 unatarajiwa kukimbizwa Wilayani Kakonko tarehe 16 Agosti, 2023 na kupokelewa Kimkoa Wilayani Kakonko uk...

MAANDALIZI YA MBIO ZA MWENGE YAANZA WILAYANI KAKONKO

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Aggrey Magwaza amefanya kikao cha kwanza cha Kamati ya maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 na kupitisha miradi itakayopitiwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru utakaokimbizwa Wilayani Kakonko tarehe 16 Agosti, 2023. Col. Aggrey Magwaza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo anayekaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko amekutana na wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko leo Mei 17, 2023. Miradi iliyopendekezwa na kupitishwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023   ni  Uzinduzi wa vyumba 08 vya madarasa na ofisi 3 za waalimu shule ya Sekondari ya wasichana Kakonko, Kutembelea kikundi cha Vijana bodaboda Muganza, Uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala kikundi cha Vijana Itumbiko, Kuweka jiwe la Msingi nyumba ya Mkuu wa Wilaya (Ikulu ndogo Kakonko) inayojengwa Itumbiko, Kukagua Barabara ya lami Kakonko-Itumbiko inayoelekea hospitali ...

TOENI HUDUMA KWA KUZINGATIA MAADILI-KANALI MAGWAZA

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Aggrey John Magwaza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo ameyahimiza Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa huduma kwa kuzingatia misingi na maadili ya kitanzania. Kanali Magwaza amesema hayo katika Warsha ya Mkutano wadau wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Wilayani Kakonko iliyofanyika Mei 16, 2023, katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Mkuu wa Wilaya ameeleza katika kipindi hiki yameibuka mashirika yanayounga mkono suala la ndoa za jinsia moja jambo ambalo si jema katika jamii za kiafrika, hivyo ameyasisitiza mashirika kutotekeleza shughuli hizo hata kama ni sehemu ya majukumu yao. Aidha katika hotuba yake ameeleza anatambua mchango mkubwa unaotolewa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na anayapongeza kwa mchango huo vile vile kuna baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali hapa nchini yamekuwa hayazingatii wajibu wao wa kisheria hivyo kusababisha malalamiko na manung’uniko kutoka kwa wananchi na baadhi ya wadau  wa ...

MKUU WA WILAYA KAKONKO AWATAKA VIJANA KUZINGATIA MAADILI.

 Na. A.C KUZENZA  Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mallasa,amewaasa vijana Wilayani Kakonko kuzingatia maadili mema yenye kulinda utu wa mtu na kuzingatia maadili ya kiafrika hususani yale ya Kitanzania. Ametoka Wito huo  Leo Ijumaa Aprili 21,2023 wakati wa Sherehe za Mahafali ya 1 ya Chuo Cha Elimu ya Ufundi Stadi JKT Kasanda, kilichopo Wilayani  Kakonko mkoani kigoma.   Akiwahutubia wahitimu hao,Kanali Mallasa,amewataka vijana hao kuyatumia mafunzo waliyoyapata chuoni hapo kutumia fursa  za miradi inayotekekezwa Wilayani Kakonko kupunguza Uhaba wa mafundi katika Fani mbali mbali jambo linalopelekea Wilaya kutafuta Mafundi Kutoka nje ya Wilaya  jambo linalo pelekea kudumaza Uchumi wa Watu wa Kakonko. "Wilaya ya Kakonko tunao uhitaji mkubwa wa mafundi  wa fani mbalimbali,hali inayopelekea kutafuta mafundi kutoka nje ya Wilaya yetu,Kwa uwepo wa chuo hiki naiona changamoto hii inakwenda kupungua" Alisema Kanali Mallasa Aidha Amewasisitiza w...

DC KIGOMA ASISITIZA MAADILI MEMA KWA JAMII

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Hamis Kali  ameendelea kutoa elimu ya Kuzingatia maadili na miiko ya  Kitanzania na kuepuka Vitendo vya ukatili    Aliyasema hayo Jana April 17, 2023 alipokuwa akihutubia Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Mtaa wa Taifa  Kata ya Rusimbi  ambapo pia alisikiliza Kerò za Wananchi pamoja na kuzitatua   Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Wazazi kuendelea kuwaelimisha Watoto Kuzingatia maadili sahihi na kuepuka Migogoro na ukatili  ndani ya familia inayosababisha ongezeko la  watoto wa mitaani  Aidha aliwataka Wananchi kuendelea kuhamasika  kulima zao la Michikichi ya Kisasa kwa lengo la kuwa na uzalishaji mkubwa na wenye tija ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na familia Alisema tayari ugawaji wa kadi za vitambulisho vya Taifa (NIDA) unafanyika kwa kila Kata kwa Wataalamu kupita kugawa kwa kuhirikiana na viongozi wa eneo husika  Naye Diwani wa Kata ya Rusimbi Mhe. Bakari Songoro akiishukuru Serikali y...