Skip to main content

Posts

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KAKONKO.

  Katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji Wilayani Kakonko,kaimu katibu tawala wa Wilaya Kakonko Bw.Aman Alexander, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Malasa,amewaongoza wananchi wa Kijiji Cha Nyakayenzi kilichopo kata ya Kasuga wilayani Kakonko kupanda miti katika chanzo cha maji Nyakayenzi,leo Tarehe 21,Machi,2023. Akizungumza wakati wa zoezi hilo kaimu katibu tawala Bw.Alexander amewasisitiza viongozi wa vijiji kupitia kamati za maendeleo, kuendelea kuwahamasisha wananchi kupanda miti hasa katika vyanzo vya maji Ili kivilinda vyanzo hivyo Pamoja na kukabiliana na mabadiliko tabia nchi. "Viongozi tushirikiane kupanda miti rafiki katika  vyanzo vya maji.. Ili kivitunza vyanzo hivi vya maji ,pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi" Aidha Bw.Alexander amewaomba wananchi kukubali kupokea miradi mbali mbali inayoletwa kutekelezwa katika vijiji vyao na waitunze kwani miradi hiyo ndiyo inayochochea maendeleo yanayokusudiwa na Serikali. Kwa upande mwi...

KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2023.

  Mkoani Kigoma maadhimisho hayo yamefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya  Kigoma vijijini ambapo wanawake kutoka Taasisi mbalimbali, wataalam pamoja na wajasiriamali wameshiriki kilele cha maadhimisho hayo. Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Thobias Andengenye alikua mgeni Rasmi. Cc @kigomars @ Kigoma Press Club Kgpc

MAAFISA UGANI KUANZA KUWAFIKIA WAKULIMA MOJA KWA MOJA

  Maafisa Ugani wilayani kibondo mkoani kigoma , wamesema kwa sasa wataanza kutumia mbinu ya kumfikia mkulima mmoja mmoja ili kuongeza tija katika kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo . Wamesema hayo baada ya kukabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kuwawezesha kuwatembelea wakulima na kuwashauri njia na mbinu Bora  za kilimo ili kufikia azima ya serikali ya sekta ya kilimo kuchangia asilimia kumi ya pato la Taifa ifikapo 2030. Wamesema awali walikuwa wakitumia mbinua ya shamba darasa kuwafundisha wakulima kutokana na kukosa usafiri lakini kwa sasa baada ya kuwezeshwa usafiri wataweza kuwatembelea na kumfikia mkulima mmoja mmoja lengo ikiwa ni kuongeza tija katika kilimo. Mkuu wa wilaya ya Kibondo Kanali Agrey Magwaza amewaagiza Maafisa Ugani hao kuzitumia pikipiki walizopewa kuwafikia wakulima na kwamba serikali itafanya ufuatiliaji kuhakikisha pikipiki hizo zinatoa mchango katika sekta ya kilimo kupitia ushauri wa maafisa ugani kwa wakulima. Chanzo: Kigoma Press Club...

TOENI ELIMU KWA WANANCHI" KANALI MAGWAZA

  Na A .C. Kuzenza-Kibondo Mkuu wa wilaya Kibondo Kanali Aggrey John Magwaza,amewaasa viongozi toka nchini Burundi, kuendelea kuwaelimisha wananchi kuzingatia na kufuata sheria  za nchi Ili kuepuka  kukinzana na sheria. Wito huo umetolewa mapema Jana tarehe 01 March,2023 wakati muendelezo wa  vikao vya ujirani mwema kwa kamati za ulinzi na usalama baina ya nchi ya Tanzania na Burundi. Viongozi hao kutoka nchini Burundi wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Ruyigi, Bi. Tabu Emmerencinne, amemshukuru Mkuu wa Wilaya Kibondo pamoja na kamati ya ulinzi na usalama  kwa kuwapokea vizuri na kuwapa ushirikiano pamoja na ukarimu kwa kipindi chote walichokuwepo nchini. Aidha Ameongeza kwa kusema Kuwa,Ushirikiano na ukarimu huo ndiyo tafsiri halisi ya ujirani mwema miongoni mwa Nchi hizi mbili. Vilevile Bi.Emmerencinne Ameomba mataifa haya yazidi kushirikiana katika nyanja mbalimbali mathalani nyanja za kiusalama kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kubadilishana taarifa...

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WADAU WA ZAO LA CHIKICHI

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiongoza kikao kazi kilichomkutanisha na wadau wa Kilimo cha zao la chikichi mkoani Kigoma. Awali akifungua kikao hicho, Waziri Mkuu amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kufanya Tathimini ya Mafanikio yaliyofikiwa katika kuibua, kuendeleza na kuboresha kilimo cha zao la chikichi mkoani Kigoma Kikao kazi hicho kinafanyika katika Ukumbi wa NSSF Manispaa ya Kigoma-Ujiji na kuwakutanisha Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, wazalishaji wa mbegu za chikichi, wamiliki wa viwanda vidogo vya kuchakata zao hilo pamoja na wakulima wakubwa na wadogo wa chikichi mkoani hapa. CHANZO:Kigoma Press Club Kgpc

WAZIRI MKUU AZITAKA TAASISI ZA MAAFA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU

  Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa amezitaka sekta zote zinazohusika na utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa maafa, idara au taasisi zenye jukumu la kisheria la kutekeleza kazi hiyo zihakikishe zinawajibika kikamilifu katika kushughulikia vizuri pindi maafa yanapotokea. Amesema pamoja na uwepo wa sera na sheria ya usimamizi wa maafa na nyaraka alizozindua ambazo zimelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji kwa kila sekta, ushirikiano unahitajika katika kutekeleza afua za ustahimilivu na kukabiliana na maafa. Ameyasema hayo (Alhamisi, Februari 9, 2023) wakati akizindua nyaraka za usimamizi wa maafa katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. Nyaraka zilizozinduliwa ni Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na kukabiliana na Maafa (2022). Nyaraka nyingine ni Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano Wakati wa Maafa (2022), Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja (2022-2027), Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (2022-2027) na Mwongozo wa Taifa wa Kupambana na Vitendo vya Kihali...