Skip to main content

Posts

USISEME HAYANIHUSU....

  Watu wengi Katika Jamii Huwa hawajishugulishi na Jambo lolote Ikiwa tu limetokea Katika Jamii naJambo hilo kuonekana kutowagusa Moja kwa Moja. Hali hii Mara Zote hutegemea na tabaka la Jamii,mtu/Watu, Imani na pengine Mazingira Jamii iliyopo,Ikilinganishwa na Jambo husika lililotokea. Wakati nikiwa Mdogo baba na mama yangu walikua wakinieleza Tena kwa vitendo juu ya dhana hii ya kujisemea HAYANIHUSU,Kuna Siku nlikua nikitembea na baba kuelekea shambani Mara njiani  tukakuta Mti Mdogo umeanguka njiani nilifika na kuvuka lakini Baba Yangu Akaniita na kunambia hii si Tabia njema,Maana Njia hii inatumiwa na Watu wengi ndiyo tutakayo tumia kurudi Nyumbani,Na Hatujui tutarudi Kukiwa bado na mwangaza au Usiku ukiwa umeingia, Mti Huu waweza kumuumiza mmoja wetu au watumiaji wengine wa Njia hii... Ukiutoa na Kuweka kando utaonesha kuwa Unawajali na wengine. nikapata Funzo na tangu Siku hiyo  Nikajikuta nikikuta kitu Njiani kinacho weza Leta Madhara kwangu na Watu wengine siwez k...

MWANANCHI UMEJIANDAA KUHESABIWA?

  Tangu Zama za kale Jamii Mbalimbali zilijiwekea utaratibu Wa kuhesabu Watu wake ili kubaini Idadi Yao na kuweza  kuwapatia Mahitaji Yao ya Msingi na kugawanya Rasilimali za Jamii kwa Usawa. Hata  moja ya Vitabu vya iman imeeleza Namna Jamii ya Watu Wa  walivyo weza kutekeleza zoezi la kuhesabiana ili kutambuana Kichwa kwa Kichwa Nyumba kwa Nyumba,ili Kuwa watambua Jamii ya ile Baada ya kutoka uhamishoni Misri. Uthibitisho wa Jambo Hili unaweza soma Katika Biblia Katika kitabu Cha  Hesabu 1:2-3 Tanzania ikiwa Miongoni mwa Jamii iliyo Chini ya Dunia nayo imefuata utaratibu huu wa kuhesabiana Kama ilivyo fanyika hata Katika Jamii za kale Tangu Zama za Kale. Sensa si zoezi geni hapa nchini Tanzania Kwani Miaka kadhaa iliyopita limefanyika, sensa ya kwanza ikiwa Ni Mwaka 1967, nakufuatiwa nazoezi la Sensa nyingine Kati ya mwaka 1978,1988, 2002 Na sensa ya Mwisho ilifanyika Agost, 2012. Sensa itakayo fanyika Mapema Agosti 23,2022 itakua Ni sensa ya Sita Tangu Tanzan...

HONGERA WANAWAKE

  Picha na East African Television(EATV) Na Anthonius-Kuzenza Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Mwigulu Lameck Nchemba Amewapongeza wanawake wote nchini kwa Uaminifu wao katika kurejesha Mikopo. Waziri Dk.Mwigulu Aliyasema Hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadilio ya Bajeti kuu ya Serikali mapema mwanzoni mwa Juma Hili Juni 14,2022. "Niwapongeze sana  wanawake, taarifa za kitafiti nilizopewa  zinaonesha wanawake wengi wanajitahidi  kurejesha mikopo kwa uaminifu" Picha kwa HISANI ya UN news Aidha Dk.Mwigulu Aliongeza pia Mikopo inayokopwa na wanawake Maranyingi hutumika kwa kazi iliyokisudiwa, Ikilinganishwa na Ile Mikopo inayochukuliwa na Wanaume, Ambao urejeshaji wa Mikopo kwa wanaume Huwa unasuasua Ikilinganishwa na Wanawake. "Hata mikopo ya familia kama imekopwa na wanawake, mingi huwa inafanya kazi iliyokusudiwa na hivyo inarejeshwa kwa uaminifu kuliko iliyokopwa na wanaume wengi ambao huwa hawarejeshi" Hata hivyo Dk.Mwigulu Ametoa wito kwa Watu Wote ...

BAJETI KULETA UNAFUU WA MAFUTA.

  Katika kuhakikisha Serikali inaleta unafuu wa Maisha Kwa Wananchi wake Pamoja na kudhibiti mfumuko wa Bei za Bidhaa na huduma nchini,Serikali inatarajia kupunguza ushuru wa Forodha Kwa Bidhaa za Mafuta ya Petroli nchini. Hayo Yamesemwa Mapema Jana na Waziri wa Fedha na Mipango,Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba Wakati Wa Uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti Ya mapato na matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/23,Bungeni Dodoma Juni 14,2022. Waziri Mwigulu Ameeleza kuwa Uamizi huu umefikiwa na Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki,Ambapo Ushuru wa Forodha kwa Nchi wanachama utashuka Kutoka asilimia 25 Ya Sasa  Hadi kufikia asilimia 10 kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. Hii imelenga kutoa unafuu na kuwalinda watumiaji wa Bidhaa za Mafuta ya Petroli. "Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwenye mafuta mengineyo ya petroli yanayotambulika kwa HS Code 2710.19.10. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu na...

TASAF KUWANUFAISHA WANAFUNZI WANAOTOKA FAMILIA DUNI.

  Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023,Inatarajia Kuanzisha Program Maalumu ya Kusaidia watoto wanaotoka Katika Familia maskini Ili Kukabiliana na Utoro unaopelekea Watoto kuacha shule. Tamko hilo limetolewa leo na Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Mwigulu Lameck Nchemba,Wakati Wa Kuwasilisha bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/23,Mapema leo Juni 14,2022 Bungeni Dodoma. Dr.Mwigulu Ameeleza kuwa Serikali imefikia Uamizi huo kufuatua watoto Wengi kukatisha Masomo Yao kutokana na Sababu Mbalimbali ikiwemo umasikini wa Kipato. Hivyo serikali Kupitia mfuko wa kunusuru kaya maskini TASAF,Imekusudia Kuanzisha Dirisha mahususi (Special Fund) Kwaajiri ya kuwahudumia Watoto wanaotoka kaya maskini Ili kuwawezesha kuhudhuria masomo, Serikali imeonesha nia hiyo kwa kutenga kiasi Cha Tsh.Bilioni 8 Kwaajiri ya Watoto wanaotoka Familia maskini Katika Mwaka huu wa Fedha. "Ili kukabiliana na  utoro (drop out) wa wanafunzi wanaotoka  familia ma...

RAISI SAMIA AWAPONGEZA SERENGETI GIRLS..

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hasani,Ameipongeza timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 Serengeti Girls Kwa Kufuzu kushiriki mashindano ya kombe la Dunia wanawake chini ya miaka 17 Yanayotarajia Kufanyika nchini India  Mwezi Oktoba. Mhe.Rais Samia kupitia ukarasa wake wa mtandao wa twita ameandika "Nawapa Pongezi Timu ya Taifa ya Soka la Wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022. Hongera kwa benchi la ufundi na wote waliochangia kufikia hatua hii. Mmeweka historia kubwa na adhimu kwa nchi yetu. Ninyi ni fahari ya Watanzania". Kwa Upande mwingine Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akiwa bungeni Mapema leo Juni 6,2022 Ameipongeza timu Hiyo ya wanawake  na amewapongeza wanawake wote nchini Kwa heshima wanayo endelea kuiletea Nchi Yetu katika nyanja mbalimbali. "Hongereni Sana Serengeti Girls, Hongera Sana Mhe. Rais, Hongereni sana Wanawake wote wa Tanzania, hakika mmetuheshimisha,...

CDF JENERALI MABEYO KUSTAFU MWISHONI MWA JUNI,2022

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwa kutekeleza vema majukumu yake katika kipindi chake chote cha utumishi ndani ya Jeshi hilo. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo alipozungumza na Jenerali Mabeyo ambaye alifika Ikulu Zanzibar kumuaga Rais kufuatia kumaliza muda wa utumishi wake ndani ya Jeshi mwisho wa mwezi wa sita kwa mujibu wa sheria. Jenerali Mabeyo alisema Jeshi la Ulinzi Tanzania litaendelea kumkumbuka Rais Dk. Mwinyi kwa busara na hekima zake katika kuzishughulikia changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi hilo ambalo hatimae limepata mafanikio makubwa. 📆 06 Juni, 2022 Ikulu,Zanzibar https://t.co/pZ9ofb94ui #Lucas Ambrose Mboje